Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum
Publication Date
2022-06

Tangu mwanzo wa historia, umaskini na unyonge umetambuliwa kuwa changamoto na vikwazo vikuu vya maendeleo ya binadamu na jamii ya binadamu. Miongoni mwa mambo haya ni suala la mali, utengenezaji mali, umililki wake, usambazaji na mtazamo wetu kuhusu mali.

Mafundisho ya kithiolojia yanatuambia kwamba binadamu wote wameumbwa kwa Mfano wa Mungu. Kwake, sisi tunatoshana. Lakini tunaona kwamba tofauti kati ya matajiri na maskini katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na kusini mwa Afrika, zinaongezeka kwa kasi. Watu wachache wanazidi ‘kufanikiwa’ na ‘kutajirika’ huku idadi kubwa ya watu ikizidi kuwa maskini zaidi. Ajabu ni kwamba, haya yanatokea katika ulimwengu ambao Mungu ameubariki kwa wingi, kiasi cha kuruhusu kila nafsi hai duniani kuwa na maisha ya yenye hadhi na starehe. Mahatma Gandhi aliwahi kusema: ‘Dunia ina uwezo wa kukidhi mahitaji ya kila mtu, ila si uchoyo wa kila mtu’.

Kama wawakilishi wa Mungu duniani, wanadamu ni wasimamizi wa uumbaji, ambao wanapaswa kuutumia kuendeleza manufaa ya umma. Lakini tumeasi mwongozo wa kiungu na kuchukua mifumo ya ubinafsi na inayoendeleza kupenda mali. Mifumo inayowatuza tabia ya kula rushwa, ubashiri na uvivu na kudunisha ya uchapakazi, uvumbuzi na ubunifu. Mifumo ambayo inajivunia kuwafanya baadhi ya watu kuwadhalilisha wengine, kudumisha utumwa mamboleo. Mfumo wa kiuchumi wa leo unaufanya ukosefu wa usawa kukita mizizi, huku ukiwawezesha watu wachache kujlimbuikizia mali na kuwalazimisha mamilioni ya watu kuishi katika uchochole. Kukosekana kwa usawa kunachochea umaskini. Kunachochea vurugu na ukosefu wa usalama. Kunawanyima mamilioni ya watu haki yao ya kuishi maisha kamili yenye hadhi. Ukosefu wa usawa unatatiza jamii zetu kama tunavyozifahamu leo.

Attachment Size
Ukosefu wa Usawa.pdf (5.76 MB) 5.76 MB