Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

WAJIBU – Institute of Public Accountability ni taasisi isiyo ya iserikali iliyosajiliwa kwa mjujibu wa sheria ya AZAKI Na. 24 ya mwaka 2002 ikiwa na namba ya usajili 00056. WAJIBU ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kukuza mazingira ya uwajibikaji nchini Tanzania.

Waanzilishi wa WAJIBU wanaamini kuwa ushirikiano na Serikali katika kukuza uwajibikaji wa kifedha ni muhimu sana. Na ushirikiano huu utawezekana kama nchi itaufanya uwajibikaji kuwa ajenda ambayo itakuwa inajadiliwa na wananchi wa kawaida. Wananchi wanatakiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuelewa na kudai uwajibikaji kutoka kwa watendaji wa Serikali.

Kazi ziinazofanywa na WAJIBU:

WAJIBU inafanya kazi kwa kuzalisha taarifa za uwajibikaji ambazo zimerahisishwa na kuzisambaza kwa wananchi wa kawaida kupitia AZAKI zilizopo katika maeneo yao. Vilevile, WAJIBU inawajengea uwezo wadau mbalimbali juu ya masuala ya uwajibikaji, wadau hawa ni kama vile vyombo vya habari, Taasisi za Elimu ya Juu, Watendaji wa Serikali, Wawakilishi wa Wananchi pamoja na AZAKI zilizopo katika ngazi za nchini.

Katika kutekeleza majukumu yake, WAJIBU inashirikiana na Serikali kupitia taasisi zake, AZAKI pamoja na kamati za usimamizi za Bunge. Ili kufanikisha malengo yake ya kukuza uwajibikaji nchini, WAJIBU inapata msaada wa kifedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ambao ni; UKAID, GIZ, Foundation for Civil Society, Hivos, Ubalozi wa Canada nchini Tanzania na Twaweza East Africa.

-6.7815713272312, 39.268763738533