Ndugu Terry ni mtaalamu wa Biashara ya Kilimo na Mtaalamu wa Sayansi ya Chakula mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi na mitano, akifanya kazi zaidi na mashirika ya wanachama ya ngazi ya juu, yakiwemo Baraza la Nafaka Afrika Mashariki (EAGC), Baraza la Mchele Tanzania (RCT), Mtandao wa Mimea Jamii ya Kunde Tanzania (TPN), Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA) na Chama cha wasindikaji wa bidhaa za maziwa Tanzania (TAMPA). Ana uzoefu mpana katika masuala yanayohusiana na kukuza mifumo rasmi ya biashara na kuunda mazingira wezeshi ya biashara kwa wakulima wadogo na makampuni ya biashara ya kilimo. Katika muda wake wote wa kazi, Bw. Terry amekuwa mtaalamu muhimu katika kuboresha mifumo rasmi ya biashara na kutekeleza programu za maendeleo ya kilimo, zenye lengo la kufungua fursa kwa biashara ndogo na za kati kukua na hatimaye kuchangia katika kuongeza pato la taifa. Ana uhusiano mzuri wa kikazi na wadau mbalimbali wa kilimo, kuanzia viongozi wa juu wa serikali hadi wakulima wadogo vijijini.
Bw. Terry pia ana uzoefu mzuri wa biashara ya kilimo na watoa huduma katika Kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko. Amehusika katika miradi kadhaa ya kitaifa ya kukuza minyororo ya thamani ya Alizeti, Kunde, Soya na Nafaka nchini Tanzania. Katika maendeleo ya taaluma yake, Bw. Terry amejijengea uzoefu mkubwa katika kusimamia miradi inayofadhiliwa na wafadhili, ikiwemo USAID, USDA, UKAID, EU, SIDA, Rikolto, FAO, ITC na AGRA.