Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Hakikazi Catalyst ni shirika linalijihusisha na uchechemuzi wa haki za kiuchumi na kijamii za Kitanzania zilizo Jijini Arusha. Tangu 2000, tumeanzisha njia mpya ya kufanya kazi na tunaamini maarifa yanaweza kuchochea hatua kwa mabadiliko kiuchumi na kijamii.

Miongozo ni zana muhimu za sehemu ya kwanza ya mkakati wetu, ambayo inakusudia kuhamasisha watu kujifunza na kujishughulisha na sera zinazoathiri maisha yao. Katika kutengeneza miongozo tunakusudia kuhudumia wigo mpana wa wasomaji.

Pia tunafanya kazi na jamii ili kuimarisha uongozi na uelewa wa pamoja wa athari za sera katika maisha. Hii ni pamoja na kuwasilisha maoni ya jamii katika michakato ya maamuzi katika ngazi ya mitaa na kitaifa, kukuza utamaduni wa kushiriki na uwajibikaji, na kuhimiza hatua za mabadiliko.

-3.3796743857429, 36.655324847979