Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linafanya kazi ya kuwawezesha wanawake kupata haki zao na kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu walio katika mazingira magumu nchini Tanzania.

Kazi zinazofanywa na WLAC:

Msaada wa kisheria

Utoaji wa huduma za kisheria zinazopatikana kwa hali ya juu kwa wanawake na watoto walio katika mazingira magumu ni msingi wa dhamira ya WLAC. Wanawake na watoto wameathiriwa sana na umaskini, na utoaji wa huduma za kisheria za WLAC hushughulikia hili moja kwa moja kwa kuwawezesha kupata fursa za kumiliki ardhi na uchumi ambazo wananyimwa mara kwa mara kwa sababu ya mila na maadili ya kitamaduni.

Uchechemuzi

WLAC inaamini kuwa kwa kushirikiana na mashirika yenye nia moja, inaweza kuimarisha uwezo wake wa kuboresha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto na kuimarisha usawa wa kijinsia nchini Tanzania. Kwa sababu hii, lengo la kimkakati la WLAC ni kushawishi na kutetea mabadiliko yanayofaa katika sera zinazohusu haki za wanawake na watoto.

-6.7906350558701, 39.266222638533