Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Tumefanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini, kujenga jamii zenye afya, kuimarisha mifumo ya elimu-jumuishi, na kusaidia watu kuwa na maisha. Hivi sasa tunafanya kazi katika mikoa saba Tanzania Bara, na pia Zanzibar.

Kazi zinazofanywa na VSO Tanzania: 

Jamii zenye afya

Katika Mkoa wa Lindi, moja ya mikoa yenye viwango vya juu zaidi vya ujauzito wa vijana nchini, timu za vijana wa kujitolea zinatumia mchanganyiko wa ubunifu wa maigizo na ujifunzaji shirikishi ili kuwaelemisha wasichana.

Elimu Jumuishi

Mpango wetu wa Elimu Jumuishi unazingatia shule za awali na za msingi, kufanya kazi ya kuwawezesha watoto wote kupata elimu bora ambayo inawaruhusu kufikia uwezo wao.

Tunazingatia vijana waliopembezoni zaidi, haswa wale wanaoishi na ulemavu, wale walio katika hali za shida, na wasichana. Tunafanya kazi kukuza maarifa na ujuzi wa waalimu katika ujifunzaji unaozingatia mahitaji ya watoto, kuboresha usimamizi wa shule, kuhimiza msaada wa jamii kwa shule za mitaa, na kukuza mifumo kamili ya ulinzi wa watoto.

-6.7590744576795, 39.24554991639