Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni katiba iliyotungwa mwaka 1977. Katiba hii inaielezea Tanzania kama nchi ya kidemokrasia, inayofuata misingi na haki za binadamu na siasa yake ni ya vyama vingi. Katiba ni sheria mama ya nchi inayowawezesha wananchi kujitambua kama taifa na ya kiutawala inayoelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola. Ibara ya 6 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa maana ya neno “Serikali” ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali za Mitaa na mtu yoyote anayefanya kazi kwa niaba ya serikali.
Pamoja na kwamba Serikali za Mitaa zinatambulika na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama inavyoeleza muundo na kazi za serikali hii katika ibara ya 145 na 146 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano, bado muundo na utekelezaji wa serikali hii si huru kama zilivyo serikali nyingine hususani Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na hatimaye kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kwa uzoefu tulionao na baada ya kusoma kwa makini katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na Sheria za Serikali za Mitaa (1982 toleo la mwaka 2002) tumegundua ya kwamba zipo changamoto na matatizo ya dhahiri yanayofifisha ufanisi wa Serikali za Mitaa. Hii ni pamoja na utata wa kimuundo, kuingiliwa kimaamuzi, uwalakini kwenye mipango shirikishi na kutokuwa huru kwenye Mapato na Matumizi ya Rasilimali. Chapisho hili basi limeandaliwa kuainisha mapungufu yaliyomo katika katiba ya sasa yanayominya uhuru wa Serikali za Mitaa katika utendaji wa kazi zake na kutoa mapendekezo yatakayochangia kwenye mjadala wa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya. Kusoma soma kiambatanisho hapa chini

KatibaLGWG.pdf (332.21 KB)