Mchango wa Redio ya Jamii katika Kutatua Changamoto za Afya, Newala
Policy Forum (PF) ni mtandao wenye muunganiko wa zaidi ya asasi za kiraia 60 ulioanzishwa mwaka 2003 kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanachama wa PF wana malengo ya kuhamasisha utungwaji wa sera zenye kulenga kupunguza umaskini, kuleta uwajibikaji katika fedha za umma kuanzia ngazi ya chini hadi Serikali Kuu.
PF pamoja na malengo yake mengine, ni kuchochea uboreshwaji wa huduma za kijamii, kupitia uwongozi bora wenye kuwajibika kwa matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Lakini pia kutumia njia mbalimbali za kuhamasisha wananchi kama vile redio katika kujitolea na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za kijamii. Pia vipindi hivi vya PF vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu michaka[1]to ya sera na namna wananchi wanavyoweza kushiriki kwenye michakato hiyo kujiletea matokeo chanya.
Vipindi hivi vinamchango mkubwa kwenye jamii mbalimbali na vimewezesha wananchi wa maeneo husika kuelezea changamoto wanazokumbana nazo na namna ya kushiriki katika kujitolea ili kukabiliana na chan[1]gamoto hizo. Mfano mmojawapo wa redio iliyoweza kuleta matokeo chanya kwenye jamii ni Redio Safari iliyopo Mtwara, ambayo ilitoa hamasa kwa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Mojawapo ya vipindi vya Policy Forum vilivyorushwa na redio hii kuanzia mwaka 2019 na kuleta mabadiliko katika jamii ni vipindi vilivyohusu changamoto za ukosefu wa huduma za afya wilayani Newala katika mkoa wa Mtwara.
Vipindi hivi vilihamasisha wananchi kujenga Zahanati katika kijiji chao cha Moneka, ikiwa ni Zahanati ya kwanza kijiji hapo tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961. Kabla ya ujenzi wa Zahanati hiyo, wananchi wa kijiji cha Moneka walikuwa wanasafiri hadi Newala mjini kuta[1]futa huduma za afya kama vile huduma za afya ya uzazi. Jitihada za wananchi zilipelekea kijiji, Mbunge wa jimbo la kijiji hicho pamoja na serikali kutoa mchango wa kumalizia Zahanati hiyo pamoja na nyumba ya Mganga Mkuu, baada ya hamasa iliyofanywa na kipindi cha PF kinachoitwa Kusini na Maendeleo kinachotangazwa kupitia Redio Safari. Pakua taarifa kamili hapo chini.