Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

 

Policy Forum ilichagua Bodi yake mpya ya Wakurugenzi wakati wa Mkutano wake wa mwaka wa 2012 uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 4 wa mwezi Mei. Wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao, ni Julie Adkins wa SNV Tanzania, Esther Mongi wa World Vision Tanzania, Emmanuel Kallonga wa Hakikazi Catalyst na Kellen Mngoya wa HAFOTA , hao ndio waliostaafu katika mkutano huu mkuu wa mwaka na kuwaacha nyuma Sr Rita Toutant-The Tanzania Network of Community Health Funds (TNCHF), Ben Taylor - Daraja na Audax Rukonge- Agricultural Non State Actors' Forum  (ANSAF) kukaa kwa mwaka mwingine ili kuwe na uwiano kati ya uingizwaji na mwendelezo wa Bodi.

Katika hotuba yao ya kuondoka waliwashukuru wanachama wa PF kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kutumika katika bodi na ushirikiano wao wakati wa uongozi wao na waliwatakia Bodi mpya ya Wakurugenzi kila la kheri katika kufanyia kazi nzuri ya mtandao na kuiongoza Sekretarieti.

Wajumbe Wapya wa Bodi

1. Aida Kiangi - ActionAid Tanzania
2. Godfrey wawa-Forum Syd
3. Hellen Kijo-Bisimba – Legal and Human Rights Centre
4. Nemence Iriya / Asia Lembariti - MACSNET

Wajumbe wa Bodi wanaokaa kwa mwaka mwingine

5. Sr Rita Toutant - The Tanzania Network of Community Health Funds Jamii (TNCHF)
6. Ben Taylor - Daraja
7. Audax Rukonge - Agricultural Non State Actors' Forum  (ANSAF)