Ikishirikiana na Mwanza Policy Initiative (MPI), wiki hii Policy Forum inaendesha warsha kuhusu Uwajibikaji Jamii (Social Accountability Monitoring – au kwa kifupi, SAM) kwa ajili ya asasi za kiraia za Mwanza.
Warsha hii imeanza tarehe 28 Julai hadi Agosti Mosi na ni moja kati ya malengo ya Policy Forum ya kusaidia kuboresha uwezo wa asasi za kiraia kuelewa, kufuatilia, kushiriki kwa ufanisi, na kushawishi michakato ya sera za kitaifa na zile za ngazi ya serikali za mitaa.
MPI ilichaguliwa na wanachama wa PF kuwa moja ya mitandao itakayofanya kazi pamoja na Policy Forum kutekeleza SAM. Warsha hii inakuja baada ya nyingine iliyofanyika Kibaha kwa ajili ya asasi za kiraia za wilaya hiyo (tarehe 21-24 July) ili kuzitayarisha ziweze kushiriki kwenye zoezi la kufuatilia uwajibikaji Kibaha. Mpango huu unasimamiwa na kikundi-kazi cha bajeti kikishirikiana na kikundi-kazi cha serikali za mitaa, vyote vikiwa chini ya mtandao wa PF.
Ni matumaini kuwa warsha hizi zitasaidia mitandao na wanachama wao kujenga uwezo katika kuchambua sera na ushawishi. Warsha ya SAM itafuatiwa na PF kutembelea wanachama wa MPI ili kujionea kwa karibu jinsi wanavyofanya kazi na kupata kuelewa juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi za ushawishi.
Kabla ya warsha hii kuanza, washiriki waliulizwa wanategemea kunufaikaje kwa kushiriki kwao. Walisema yafuatayo:
- kuongeza uelewa wa SAM
- kujua SAM inatumikaje
- Kujua mbinu mpya za kufuatilia uwajibikaji katika taasisi za nchi yetu
- Kupata chachu itakayosaidia kuhamasisha wengine
- Jinsi ya kufikisha uwajibikaji maeneo maalum
Muhtasari wa siku ya nne
Muhtasari wa siku ya tano