Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Policy Forum inapenda kuwatangazia wanachama wake kuwa mkutano mkuu wa mwaka 2010 utafanyika tarehe 12 na 13 Aprili. Mahali patakuwa ni Blue Pearl hotel in Ubungo kuanzia saa 3 asubuhi. Wanachama watatumiwa mwaliko rasmi pamoja na nyaraka zote muhimu siku saba kabla ya mkutano. Kama kawaida yetu, shughuli za mkutano mkuu zitahusisha:

1.       Kupokea, kutathmini na kukubali mahesabu ya Policy Forum ya mwaka wa fedha unaoisha 31 Disemba 2009 pamoja na ripoti ya mwaka huo.

2.       Kuchagua wakaguzi wa mahesabu ya Policy Forum kwa mwaka wa fedha unaoisha 31 Disemba 2010.

Vile vile, kutakuwa na uchaguzi kwa ajili ya wanachama kujaza nafasi zilizopo kwenye bodi ya wakurugenzi wa Policy Forum. Hivyo, wanachama wenye uwezo na nia wanakaribishwa kuchukua fomu za maombi kutoka kwa Sekretarieti. Kutokana na katiba yetu, asilimia 50% ya wanachama waliopo kwenye bodi wanapashwa kuachia ngazi kila mkutano mkuu na watakuwa wale walioshika wadhifa kwa muda mrefu zaidi. Nafasi hizo kwa sasa ni:
 
1.       NGO ya kimataifa (kujaza nafasi iliyoachwa na Mama Rose Mushi.
2.       NGO ya kimataifa (kujaza nafasi inayoachwa na Concern Tanzania – walikuwepo kwa muda mrefu zaidi). 
3.       NGO ya Dar (kujaza nafasi iliyoachwa na TEN/MET - baada ya kufariki kwa Dr. Joseph Kisanji).
4.       NGO ya mkoani (kujaza nafasi inayoachwa na KIVULINI - walikuwepo kwa muda mrefu zaidi)