Skip to main content
Submitted by Web Master on 30 June 2015

Tarehe 16 Juni 2015 Serikali ya Tanzania  ilipeleka miswada mitatu bungeni inayohusu sekta ya uziduaji chini ya “Hati ya Dharura.”  Miswada hiyo ni Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2015 (The Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act 2015, Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015. (The Oil and Gas Revenue Management Act 2015)  Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 (The Petroleum Act 2015).

Kwa msingi huu, sisi wana Asasi za Kiraia (AZAKI)  kwa majina tajwa hapa chini tulikutana na kujadili miswada hiyo  jijini Dares Salaam kuanzia tarehe 21 hadi  23 Juni, 2015 kwa lengo la  huchambua na kuboresha  miswada ya sheria zilizopendekezwa kwa  manufaa na maslahi mapana ya taifa .

TUNAIPONGEZA sana Serikali kwa juhudi zake katika kusimamia  rasilimali hizi za taifa kimkakati kwa madhumuni ya kuleta  ufanisi na kwa manufaa ya  vizazi  vilivyopo na  vijavyo  hapa nchini.

TUNASISITIZA   ukweli  kwamba, kwa ujumla, miswada yote mitatu  ina vifungu vingi vyenye kulinda maslahi mapana ya taifa  pamoja na kuvutia uwekezaji katika  sekta  na  kuhakikisha uwazi na kuendeleza uchumi imara. 

Pamoja na hayo, tuna WASIWASI na hofu kubwa  juu ya  wakati na  haraka iliyotumika katika kuandaa na kuwasilisha Bungeni miswada hii muhimu ya sheria., ikizingatiwa kwamba imekuwa ni ada na kawaida ya serikali kuwasilisha bungeni miswada muhimu tena  kwa hati za darura kama ilivyokuwa mwaka 2010  kwa Sheria ya Madini.  Muhimu zaidi, ni kuhakikisha kuwa Serikali inaweka  sheria zilizo sahihi.katika usimamizi wa sekta husika.

TUNAWASIHI Wabunge kupitia miswada hii kwa uangalifu japokuwa  tunafahamu kuwa nguvu kubwa na mitazamo ya wabunge walio wengi kwa sasa    emeelekezwa zaidi  kwenye uchaguzi mkuu ujao na huenda ikasababisha vipaumbele na umakini katika kujadili miswada hii kupungua kwa kiasi kikubwa kama tulivyo shuhudia mahudhuriio hafifu bungeni katika mkutano wa bajeti unaoendelea

Rasimu ya Sheria ya Petroli ya mwaka, 2015

Wakati muswada unaweka muundo wa kitaasisi- ili kusimamia sekta ya petroli, unalenga kuimarisha udhibiti na weledi katika kuendesha sekta, hata hivyo kuna vifungu vinavyo sababisha kuingiliana kiutawala, Vifungu hivi kama vitapitishwa bila kurekebishwa, chuenda vikaathiri motisha na kuleta msuguano kati ya taasisi zinazopendekezwa kuanzishwa katika muswada huu. hivyo kuhatarisha usimamizi madhubuti wa  sekta ya petroli.

Matumizi neno “pekee” (exclusive) juu ya mamlaka ya Kampuni ya Taifa ya Mafuta (National Oil Company) katika vifungu 10 (2) na 45 inaweza kuleta utata katika tafsiri na kuleta changamoto kiuwajibikaji.  Wakati mfumo kama  huu unaweza kuwa na faida fulani katika kujenga uwezo wa  kampuni hiyo kujifunza biashara na kujipangia mikakati yake ya ubia bila vikwazo, kuna hatari kuwa  uchaguzi wa wabia utategemea zaidi faida za kiuchumi  za kampuni ya taifa ya mafuta(NOC) kuliko maslahi mapana ya taifa kwa ujumla. Hii ni kinyume na madhumuni ya Sera ya Taifa ya Gesi na rasimu ya Sera ya Petroli.  

Kifungu cha 6:“Kamishna wa petroli atakuwa mshauri wa Waziri kuhusu sera, mipango na kanuni pamoja na masuala ya utawala ya siku hadi siku katika sekta ya petroli na sekta ndogo ya gesi.”

Wasiwasi / Mashaka: Kuunda nafasi ya kamishna wa petroli ambaye atakuwa katika nafasi  sawa na kamishna wa nishati kunaweza kuleta muingiliano/mgongano katika majukumu,  lakini kisera na kitaalamu petroli kama bidhaa iko  chini ya sekta ya Nishati.

Tunapendekeza: Kuunda nafasi za Naibu Kamishna wa nishati anayeshugulikia maswala ya Petroli akiwa na wajibu /majukumu mahususi ya kusimamia sekta ya Petroli na/au Nishati kwani kuna umuhimu wakuimarisha ofisi ya Kamishna wa Nishati kwajili ya kuondoa muingiliano na mgongano wa kiutendaji.

Kifungu 45: “Kampuni yaTaifa ya Mafuta itakuwa na “haki ya pekee” katika uchimbaji wa  mafuta chini ya  Sehemu hii.”

Wasiwasi: vifungu hivi viwili vinapingana  na Kifungu 45 (4)  kinachoelezea mgawo/hisa kwa  kampuni yaTaifa ya  Mafuta (NOC)  na kifungu 219 (1) ambacho kinaipa  serikali uwezo wa   kuamua mgawo/hisa  hivyo   kuibua changamoto za kiuwajibikaji pamoja na urasimu a wa kitaasisi.

Tunapendekeza: Haki ya pekee kwa kampuni ya taifa ya mafuta(NOC)iwekewe sharti la kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kifungu  101 (3): “ Mwenye leseni na mkandarasi  hawatachoma gesi au kucheu na kumwaga  mafuta  bila ruhusa ya awali toka kwa  PURA.”

Tuna wasiwasi;  kwamba sheria inayopendekezwa  inaifanya PURA kuwa na uamuzi wa mwisho bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mamlaka za usimamizi wa mazingira kama Tume ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC).  

Tunashauri:  Waziri awe na mamlaka ya mwisho ya utoaji  kibali cha kuchoma gesi au kucheua mafuta baada ya kupata ushauri wa kimaandishi kutoka PURA na NEMC.

Zaidi ya hayo, ni muhimu sana kwamba muswada huu kuweka vipengele vinavyolazimisha uchapishaji wa taarifa muhimu  ili kuongeza uwazi wa sekta ya mafutana gesi.  Taarifa hizi zijumuishe: Taratibu za utoaji zabuni ikiwemovigezo vya kushiriki na  kushinda zabuni hizo, orodha ya makampuni yanayoweza kushiriki, vigezo vya kupata mshindi , orodha ya washindani, washindi wa zabuni, taarifa ya tathmini ya o wa zabuni ikithibitisha ushindi ulivyopatikana na vigezo vilivyotumika. Pia taarifa ya Mikataba yenye maelezo yote, pamoja na marekebisho na viambatanisho vyake,   na mnufaikaji kutokana na umiliki wa  leseni (beneficial ownership of license holders), matokeo ya tathmini  ya kimazingira,   mipango ya usimamizi wa mazingira, na taarifa za mwaka na mipango ya kuendeleza  unufaikaji kwa wananchi

1.1  Muswada wa Sheria yaUsimamizi wa Mapato ya Mafuta  na Gesi wa Mwaka 2015

Muswada wa Sheria inayopendekezwa una vipengele muhimu sana kuhakikisha usimamizi makini wa mapato yanayotokana nauchimbaji  wa mafuta  na gesi;  kuendeleza uimara wa fedha na uchumi mkuu na kupanga mikakati ya uwekezaji  sambamba  na vipaumbele vya  mipango ya maendeleo ya muda wa kati na muda mrefu, hivyo kuleta maendeleo endelevu.   Lakini, kanuni / taratibu za fedha zilizopendekezwa  hazihakikishi   haki sawa  baina ya vizazi  kwa maana ya kuweka akiba  sehemu ya  mapato kwa ajili ya vizazi vijavyo kama ilivyo katika Sera ya Taifa ya Gesi Asilia  ya mwaka  2013.

Kuweka ukomo  wa utengaji fedha kwa ajili ya matumizi ya  maendeleo kwa kiwango cha 60% ya fedha  zilizohawilishwa kwenye akaunti ya jumla kunaweza  kuathiri  mahitaji ya uwekezaji kama huo wakati   uwezo wa kutumia utakaporuhusu  matumizi ya hadi100%  au zaidi  ya fedha zilizohawilishwa kwenye akaunti ya jumla/pamoja kutoka kwenye mfuko.   Zaidi ya hayo,   sheria iliyopendekezwa  haielezi waziwazi  kuhusu marekebisho ya mapungufu ya fedha (Kifungu 17. (1)(b).  Kwa  uelewa mzuri zaidi,  kifungu hicho kinapaswa  kuboreshwa zaidi kuhakikisha kuwa marekebisho ya mapungufu ya fedha  yanatilia maanani muda wa mzunguko wa mapato   (ukiondoa mapato  yaliyodhihirika ya mafuta na gesi ) kutoka muda  huo ambapo mapato  yanafikia  walau  kiwango kilichopangwa  cha 3% ya GDP  (Zao Ghafi la Ndani / Pato la Taifa)  wakati mapato yanaposhuka  moja kwa moja chini ya kiwango  kilichopangwa.

Wakati sheria iliyopendekezwa ina lengo la kuhakikisha upatikanaji wa fedha kwa uwekezaji  wa Kampuni yaTaifa ya Mafuta  (NOC , kufunga fedha za NOC kwa kiwango cha 0.1% za GDP hakutoi uhakikisho wa mgawo wa mapato unaofaa  kwa kuzingatia malengo yake na/au  uwezo wake wa kimatumizi.  Ili kuondokana  na uwezekano wa changamoto ya ama kutoa fedha kidogo au zaidi kwa NOC,  serikali  inaweza kufikiria kutoa fedha kwa kupitia  Akaunti  ya Jumla/Pamoja (Consolidated Account) kwa  kutegemea mipango ya uwekezaji ya  NOC ya muda wa kati na ya muda mrefu.

1.2  Sheria ya Tasnia vya Uziduaji (Uwazi na Uwajibikaji)  ya Mwaka 2015

Tunaamini kuwa sheria iliyopendekezwa itaimarisha maazimio ya Tanzania ya  kuongeza uwazi wa mapato  yaliyoanza kwa kujiunga na EITI  (Global Movement) mwaka 2009.  Tunaona kuwa tangu hapo kikundi tekelezi cha TEITI kimeendeshwa kwa kutumia hati za Makubaliano (Memorandum of Understanding),  bila kuwepo kwa  sheria zozote.  Sheria inayopendekezwa itatoa msingi wa kisheria  kwa kuhakikisha utekelezaji wa maazimio  kama inavyoelekezwa  kwa viwango vya EITI  kimataifa sambamba na maazimio ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuimarisha uwazi katika uendeshaji wa shughuli zake.

Lakini kuna  mapungufu ya wazi katika sheria hii iliyopendekezwa  ikiwemo kuifanya kikundi tekelezi kuwa chombo au  sehemu ya taasisi za kiserikali hali itakayoikosesha uhuru. Tunaomba serikali ihakikishe kuwa  chombo cha usimamizi (TEITI MSG)  kinapewa uhuru katika kuchagua wajumbe wake, kutafuta rasilimali watu na fedha  ili kuilinda dhidi ya kuingiliwa  kisiasa..

Pamoja na  hayo,  viwango vya chini vya adhabu vilivyopendekezwa katika rasimu hii kwa watakaokosa kutoa taarifa  haviakisi thamani ya tasnia ya uziduaji na inahitaji mapitio.

Imetiwa  Sahihi na :

  1. Governance Links
  2. Policy Forum
  3. Oil, Natural Gas & Environmental Alliance (ONGEA)
  4. HakiMadini
  5. Interfaith Standing Committee on Economic Justice
  6. Governance and Economic Policy Center
  7. International Alliance of Natural Resources in Africa (IANRA)

PDF Version ya gazetini