Skip to main content
Submitted by Web Master on 8 February 2012

Policy Forum kwa kushirikiana na Kanumba the Great Films wanayo furaha kuitambulisha kwenu filamu ya Kijiji cha Tambua Haki, filamu ambayo ina lenga kuelimisha jamii juu ya utawala bora na uwajibikaji katika ngazi ya serikali za mitaa hadi kitaifa.Utambulisho huu ulifanywa tarehe 8 Februari 2012 katika hoteli ya Regenct Park.

Mr. Hebron Mwakagenda kutoka Policy Forum alisema,Kama mtandao wa mashirika ya kiraia tunaona kupunguza umaskini kuongeza usawa, kurekebisha muundo wa kidemokrasia, kuleta utawala bora na uwajibikaji ni jukumu letu sote. Hivyo moja ya eneo letu kubwa ni utawala bora katika serikali za mitaa:hii inajumuisha kuhamasisha ufuatiliaji wa madaraka katika mkoa, halmashauri na ngazi ndogo ya baraza la serikali ya halmashauri.

Aliendelea kusema, Policy Forum inaamini kwamba utawala bora na uwajibikaji ni suala la maslahi ya taifa zinazoathiri ngazi zote lakini zaidi kwa jamii ambapo wengi wanaishi. Uwazi na uwajibikaji ni maadili ambayo sisi sote tunapaswa kukuza na kuendeleza. Haki ya mwananchi ya kupata taarifa ya mapato ya nchi kama vile, ni kiasi gani serikali imetenga kwa ajili ya serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo na jinsi gani inapanga kutumia, hiyo itawawezesha kuwawajibisha maafisa wanaohusika na matumizi yake mabaya.
Hivyo basi filamu ya Kijiji cha Tambua Haki inayofadhiliwa na Policy Forum inajaribu kuonyesha jinsi mifumo na michakato ya utawala katika ngazi ya serikali ya mtaa ipo katika kiini kinacho waathiri wananchi kila siku, miundo mbinu, huduma za afya na huduma kutolewa na wahusika serikalini.

Alisema filamu ya Kijiji cha Tambua Haki inathibitisha kwamba kwa kukuza uwezo na fursa ya wananchi wa kawaida kuwa na taarifa na elimu husika kuhusu haki zao, sauti ya kudai mahitaji yao, kufuatilia mienendo ya serikali na kudai uwajibikaji na uboreshaji wa utoaji wa huduma. Hii itawezekana kama serikali inakuwa wazi kuhusu jinsi gani fedha za umma zinapatikana na kutumiwa na kama wananchi wana sauti ya kujua jinsi gani  rasilimali zao zinavyopewa kipaumbele na kutengwa.

Akamaliza kwa kusema, ukosefu wa uongozi bora mara nyingi hupunguza ufanisi wa njia ya kawaida ndani ya uwajibikaji. Kwa mfano, mifumo ya kisiasa na kisheria ya uwajibikaji mara nyingi huathirika na mamlaka yatokayo juu zaidi ya utawala wa sheria. Mfumo wa uwajibikaji wa fedha na utawala mara nyingi unakabiliwa na usimamizi dhaifu. Hata hivyo katika filamu ya Kijiji cha Tambua Haki inapigia mstari kwamba, katika hali hiyo njia za ufuatiliaji wa uwajibikaji wa kijamii zinaweza kuboresha uwajibikaji kwa  kuongezea mazoea ya kawaida na kwa kuimarisha taratibu zilizopo.

Matukio katika picha:

 Kuanzia kushoto,Hebron Mwakagenda,Kanumba na Alex Ruchyahinduru

Kanumba akionyesha mfano wa kasha la filamu