Skip to main content
Submitted by Web Master on 2 December 2022

Policy Forum (PF) ni mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) yapatayo 60 ulionzishwa mwaka 2003 na kusajiliwa chini Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002 ikiwa na usajili namba NGO/R2/00015. Policy Forum ina wanachama mbalimbali ambao hujumuika kwa pamoja wakiwa na malengo ya kushawishi michakato ya kisera ili kupunguza umasikini, kuongeza usawa na demokrasia; huku mkazo mkubwa ukiwekwa katika uwajibikaji kwenye matumizi ya fedha za umma katika ngazi ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Mabadiliko yanayotarajiwa na Policy Forum ni maboresho ya utoaji huduma kwa kuzingatia utawala bora ulioimarishwa na uwajibikaji wa matumizi ya rasilimali za umma.

Uanachama wa Mtandao wa Policy Forum ni wa hiyari na upo wazi kwa shirikika lolote lisilo la kiserikali lililo sajiliwa Tanzania bara na ambalo malengo yake yanaendana na dira, dhima na malengo ya PF kama yanavyojieleza katika Mpango Mkakati wake.

Bonyeza hapa kupakua mwongozo