Skip to main content
Submitted by Web Master on 6 October 2015

Policy Forum na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tunakuletea tena chapisho hili la tatu katika mtiririko wa machapisho yanayohusu elimu kwa umma juu ya kupambana na rushwa.
Mtakumbuka kuwa chapisho letu la kwanza la pamoja lilihusu sheria mpya namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa hapa Tanzania,

Chapisho hili linaweka wazi sheria zetu zinavyosema kuhusu makosa yarushwa katika chaguzi hapa nchini Tanzania na adhabu zinazotolewa kwa makosa husika,

Kwa kuzingatia kuwa Oktoba 2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu tunaamini chapisho hili litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wakati wa chaguzi huo muhimu.
Katika chapisho hili tumeweka anuani na simu za ofi si zote za mikoa na Wilaya za TAKUKURU ili kuwarahisishia wananchi kuweza kuwasiliana na ofi si hizi pale tatizo lolote linapojitokeza. Kusoma zaidi bofya hapa.