Skip to main content
Submitted by Web Master on 20 May 2013

Policy Forum ilichagua Bodi yake mpya ya Wakurugenzi wakati wa Mkutano wake wa mwaka wa 2012 uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 4 wa mwezi Mei. Wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao, ni Sr. Rita Toutant - The Tanzania Network of Community Health Funds (TNCHF), Ben Taylor – Daraja and Audax Rukonge- Agricultural Non State Actors' Forum (ANSAF) hao ndio waliostaafu katika mkutano huu mkuu wa mwaka na kuwaacha nyuma Aida Kiangi – ActionAid Tanzania, Godfrey Wawa- Forum Syd, Hellen Kijo-Bisimba of Legal na Human Rights Centre na Nemence Iriya/ Asia Lembariti  wa MACSNET kukaa kwa mwaka mwingine ili kuwe na uwiano kati ya uingizwaji na mwendelezo wa Bodi.

Katika hotuba yao ya kuondoka waliwashukuru wanachama wa PF kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kutumika katika bodi na ushirikiano wao wakati wa uongozi wao na waliwatakia Bodi mpya ya Wakurugenzi kila la kheri katika kufanyia kazi nzuri ya mtandao na kuiongoza Sekretarieti.

Wajumbe Wapya wa Bodi

1. Israel Ilunde-Youth Partnership Countrywide (YPC)

2. Martina M. Kabisama-SAHRINGON

3. Betty Missokia / Godfrey Boniventura - Hakielimu

Wajumbe wa Bodi wanaokaa kwa mwaka mwingine

4. Aida Kiangi – ActionAid Tanzania 
5. Godfrey Wawa- Forum Syd
6. Hellen Kijo-Bisimba – Legal and Human Rights Centre
7. Nemence Iriya/ Asia Lembariti  - MACSNET