Skip to main content
Submitted by Web Master on 14 November 2007

Katika miaka kumi iliyopita, asasi za kiraia katika nchi zaidi ya 60 duniani zimeanzisha mikakati ya kuchunguza jinsi serikali zao zinavyotumia pesa za umma. Harakati hizi zimefikia kuangalia kila hatua katika ya mchakato wa bajeti: mipango, utengaji wa mafungu, matumizi na matokeo ya matumizi. 

Afrika Mashariki hasa imekuwa ikijishughulisha na michakato ya 'ufuatiliaji pesa' za umma katika ngazi za chini hasa wilayani, kwenye kata, na vijijini. Asasi hizi hutumia mbinu mbalimbali za kutathmini matumizi ya fedha za umma na mbinu zote hizi zinaweza kunufaisha wananchi ambao hujua jinsi fedha zao zinavyotumika.  Kwa sababu mbinu hizi ni tofauti tofauti, vikundi hivi vinaweza kunufaika kwa kufundishana na kuoneshana jinsi mbinu zao zinafanikisha zoezi la ufuatiliaji pesa.

Ndiyo maana Oktoba 2007, Mradi wa kimataifa wa bajeti - International Budget Project (IBP) na Policy Forum walitayarisha Mkutano wa ufuatiliaji matumizi ya fedha za umma kwa ajili ya asasi za Afrika Mashariki mjini Arusha ambao ulifadhiliwa kwa msaada kutoka kwa Open Society Initiative of East Africa (OSIEA). Mkutano ulihudhuriwa na wawakilishi 23 participants kutoka asasi 15 za Kenya, Tanzania, Uganda, na Malawi.Wawakilishi kutoka Poverty Action Network of Civil Society (Mtandao wa kukabili umaskini nchini Ethiopia) ya Ethiopia (PANE) pia walihudhuria.

Mbali na kujifunza kutoka kwa wenzao, asasi hizi pia zilidhamiria kuunda mtandao kwa ajili ya Afrika Mashariki ili kuboresha shughuli za ufuatiliaji matumizi ya pesa za umma katika ukanda huu.

Sehemu ya kwanza ya mkutano ulihusisha ubadilishanaji mbinu, masuala ya upatikanaji wa habari, matatizo yanayowakabili wahusika katika zoezi za ufuatiliaji pesa, na mafanikio. Vilevile, wajumbe walitembelea kijiji nje kidogo ya mji wa Arusha kujionea jinsi gani mfumo wa matumizi ya kadi ya 'PIMA' unavyotumika (mbinu hii ilibuniwa na Hakikazi Catalyst, asasi iliyoko Arusha).Wakati wa ziara hiyo, wajumbe walionana na wahusika wa kamati ya ufuatiliaji huo wa pesa hapo kijijini ambao waliwaonesha matunda ya kazi yao. Pia, waliona jinsi ubao wa matangazo unavyotumika kuwataarifu na kuwajulisha wanakijiji juu ya mipango ya maendeleo na matumizi ya fedha.

Kituo cha demokrasia na utawala bora kutoka Malawi - Centre for Democracy and Good Governance (CEDGG) na Youth Agenda of Kenya, walifurahia mbinu hii ya ubao wa matangazo vijijini na wakasema wangependelea kuanzisha mfumo huu nchini kwao.Kituo cha Utafiti cha Kabarole - Kabarole Research and Resource Centre (KRC) of Uganda na CEDGG walisema wangependelea kutumia mfumo wa Hakikazi wa kutumia kadi ya 'PIMA' katika ufuatiliaji pesa.

The Uganda Debt Network (UDN) ambao hushughulikia kufuatilia matumizi ya fedha mashuleni,;Waislamu kwa Haki za Binaadamu Muslims for Human Rights (MUHURI) ya Kenya; Youth Action Volunteers (YAV) ya Tanzania na TAACC of Uganda, wote walitamka kunufaika na mkutano huu na kuonesha nia ya kushirikiana katika mtandao ulioongelewa kuundwa. Pia, walisisitiza umuhimu wa kuongeza uwezo wa wananchi kufuatilia matumizi ya fedha zao katika ngazi za chini.