Skip to main content
Submitted by Web Master on 29 June 2008

Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum (LGWG) kimechapisha tafsiri rahisi ya kanuni za utawala kijijini. Kitabu hicho kinachoitwa 'UTAWALA WA KIDEMOKRASIA KATIKA JAMII: USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA SERIKALI ZA MITAA (VITONGOJI, VIJIJI NA MITAA)', kinalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mipango ya maendeleo katika vijiji na mitaa. Kama kawaida ya Policy Forum, kitabu hiki kiko kwa lugha rahisi na katuni ili kumpa hamu msomaji na kuongeza uelewa zaidi wa ujumbe kwa kile kilichokusudiwa kufika kwa mwananchi wa kawaida.

Kitabu hiki kinapatikana katika PDF kwa kubofya hapa.