Skip to main content
Submitted by Web Master on 13 May 2008

Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum (LGWG) kimechapisha tafsiri rahisi ya kanuni za utawala kijijini. Kitabu hicho kinachoitwa 'UTAWALA WA KIDEMOKRASIA KATIKA JAMII: USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA SERIKALI ZA MITAA (VITONGOJI, VIJIJI NA MITAA)', kinalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mipango ya maendeleo katika vijiji na mitaa. Kama kawaida ya Policy Forum, kitabu hiki kiko kwa lugha rahisi na katuni ili kumpa hamu msomaji na kuongeza uelewa zaidi wa ujumbe kwa kile kilichokusudiwa kufika kwa mwananchi wa kawaida.

Kitabu hiki ni mfululizo wa pili wa kuwataka wananchi washiriki katika shughuli zao katika maeneo yao, kitabu cha kwanza kilitolewa mwaka 2005. Kinapatikana katika PDF kwa kubofya hapa.