Wanachama wa Policy Forum Kufanya ziara ya Kutembelea Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Categories

Wakati wa Mkutano wake Mkuu wa Mwaka  2014 (AGM) , Policy Forum (PF) sekretarieti  iliandaa ziara yenye dhumuni la kuwafahamisha wanachama wake  wa mikoani  juu ya kazi ya taasisi muhimu za serikali ambayo imekuwa ikifanya nayo kazi kwa karibu. Kwa mwaka 2014, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (NAO) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) walichaguliwa kwa ajili ya ziara hiyo.

Ziara hizo zilifanyika siku moja ya Mkutano Mkuu wakati wa mchana ambapo timu mbili ziliundwa , moja kutembelea NAO na wengine kutembelea CHRAGG.

Katika ofisi ya NAO, wanachama walikaribishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG ), Bw Ludovick Utouh , pamoja na timu ya usimamizi nzima. Hotuba ya ufunguzi ilitolewa na CAG na kufuatiwa na maonyesho ambayo yalikuwa na lengo la kuwafahamisha wanachama juu ya kazi za ofisi . Lengo maalum lilikuwa juu ya mpango wa Mkaguzi Mkuu wa kuendeleza ushiriki wa umma katika mchakato wa ukaguzi nchini .

Majadiliano  yenye matunda yalifanyika juu ya jinsi NAO inaweza kushirikiana kwa ufanisi zaidi na asasi za kiraia. CAG alisema kuwa ofisi yake inashukuru kufanya kazi na asasi za kiraia na inatarajia kwamba asasi za kiraia zitatangaza kazi ya ofisi yake kama vile kushinikiza kusaidia kuhakikisha kwamba mapendekezo ya ukaguzi yanafanyiwa kazi na serikali. Ilionyeshwa na CAG kuwa asasi za kiraia na wananchi wanaweza kupendekeza maeneo maalum kwa ajili ya ukaguzi maalum ili kwamba mwishoni kuwe na ongezeko la uwajibikaji kwa upande wa serikali na kwamba rasilimali za umma ni busara zitumike kufikia huduma bora.

Mkutano huo pia ulisaidia kuonyesha kwa wanachama wa mikoani mantiki ya Policy Forum ya kujiunga Kikundi kazi cha NAO cha dharula cha wadau mbalimbali ambacho kina lengo la kutafuta njia madhubuti za kuboresha maarifa na uelewa wa  NAO na upande wa watendaji (CSOs) na michango  ambayo wanaweza kufanya  katika mchakato wa ukaguzi . Zaidi, kikundi kazi kina lengo la kuendeleza makubaliano juu ya wajibu na majukumu ya asasi za kiraia na NAO kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa ukaguzi  unapatikana/unawafikia wananchi. Mkutano huo ulikuwa na umuhimu zaidi kwa  wanachama wanaofanya ufuatiliaji wa uwajibikaji katika jamii (SAM) na Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) pia  kikundi kazi kina lengo la kupendekeza njia ambazo zana hizi zinaweza kuongeza utendaji wa mchakato wa ukaguzi.

Katika ofisi ya CHRAGG, Kamishna Ali Hassan Rajab aliwakaribisha wanachama wa PF na alielezea kwamba taasisi ina sera ya mlango wa wazi hivyo  hivyo asasi za kiraia zinaweza kutembelea Tume wakati wowote.

Katika mkutano huo , Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Idara, Mheshimiwa Francis Nzuki aliwasilisha kwa wanachama muundo na historia ya kuanzishwa kwa Tume ya na alisema kuwa CHRAGG ni huru na ni taasisi ya serikali iliyoundwa kikatiba. Alieleza kazi, mafanikio, mipaka pamoja na changamoto tume inazokabiliana nazo. Changamoto kubwa iliyoainishwa kwa wanachama, ni ufinyu wa bajeti ambayo alisema ndio inayoifanya tume isifanikishe majukumu yake kwa ufanisi.

Pamoja na matatizo haya , CHRAGG na Policy Forum wamekuwa wakishirikiana ikiwa ni pamoja na kuzalisha machapisho na kuandaa midahalo ya asubuhi (breakfast talks) . Katika sherehe yamwaka 2013 walizindua pamoja chapisho la pamoja la CHRAGG - Policy Forum juu ya utawala bora kwa lengo la kuhamasisha viongozi na jamii juu ya somo, Naibu Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria , Mhe. Angellah Kairuki alisema yeye alifarijika kuhusishwa na ushirikishwaji huo ukizingatia wizara yake ilikuwa na wajibu wa masuala ya utawala bora.

Wito wote huu ulitoa nafasi kwa asasi za kiraia na taasisi hizi zaserikali kutafuta njia bora ya kufanya kazi pamoja. Pia ilikuwa fursa ya kuchangia juu ya namna ya kupeana uzoefu wa shughuli za kila pande zinaweza kusaidia taasisi kufanya kazi kwa amani na asasi za kiraia . Inatarajiwa kuwa  mambo yatakuwa mazuri na utahusisha ushirikiano endelevu kama huu.

Wakati wa kikao cha mrejesho siku iliyofuata , wajumbe wa PF walikubaliana kwamba mazungumzo yalikuwa na nguzo muhimu katika kujenga ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili za serikali na hoja muhimu kupelekea ushiriki mzuri na asasi katika mchakato wa ukaguzi kama kuendeleza umuhimu wa kuchukua mbinu ya haki za binadamu kwa uwajibikaji jamii.

Policy Forum inathamini ushirikiano na mashirika mengine kwasababu unajenga fursa kwa wanachama wake kujifunza kutoka kwa wengine na kupanua maarifa ndani ya Policy Forum. Pia ni njia ya mtandao kuendeleza malengo yake ya kimkakati na kuonyesha mshikamano na mashirika yanayofanania.

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter