Utengaji wa Bajeti Isiyotosheleza kwa Sekta ya Afya

Categories

Zaidi ya theluthi mbili ya Watanzania wanaishi vijijini na wengi wao wanategemea vituo vya afya vya Serikali kupata huduma za afya ya msingi. Wananchi wanakumbana na changamoto nyingi katika kufikia huduma za afya-kuna mlolongo wa foleni ili kupata huduma katika zahanati au vituo vya afya kutokana na upungufu wa watumishi wa afya. Pia kuna upungufu wa bidhaa muhimu za afya na vifaa tiba. Idadi kubwa ya Watanzania bado wanasafiri umbali mrefu kuweza kufikia kituo cha afya kilicho karibu, na wengi wao ni maskini
hawana uwezo wa kulipia gharama za michango ya ada za huduma ya afya.
Ni nadra wananchi kushirikishwa katika maamuzi ya mambo yanayohusu afya, hivyo kuchangia ukosefu wa ufahamu kuhusu taratibu za uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), wale wanaofahamu na waliojiandikisha kwenye CHF wanakatishwa tamaa wanapofika katika vituo vyaa afya na kuambiwa hakuna dawa, jambo linalowakatisha tamaa wengine kujiunga na mfuko huo.Kusoma zaidi bofya hapa.

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter