Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii katika Sekta ya Misitu-Kibaha na Kisarawe

Categories

Mnamo mwaka 2013, Tanzania Natural Resource Forum (TNRF), mwanachama wa Policy Forum, aliteuliwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM)  wa mtandao kushirikiana na Policy Forum kufanya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM).

Baada ya TNRF kuteuliwa, timu iliundwa na ilipewa mafunzo juu ya dhana na zana za Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii na baada ya hapo walitengeneza timu ya SAM  ya utekelezaji na eneo mahususi walilolichagua lilikuwa ni sekta ya misitu, kwa kutumia maarifa na ujuzi waliopewa katika mafunzo ya SAM waliweza kuchambua nyaraka zinazohusu misitu na walifanya utetezi kwa mambo ambayo walitaka yabadilike.

Utetezi ulipelekea Policy Forum kwa kushirikiana na Kampeni ya mama misitu (Kampeni ya TNRF) kuzalisha makalajuu ya matokeo ambayo timu ya utekelezaji ya SAM iliyagundua.Makala hiyo inalenga kukuza utawala bora katika sekta ya misitu.

Bonyeza hapa kuiona makala hiyo: http://youtu.be/PfONN04Cxlk

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter