Skip to main content
Nicholas Lekule
Meneja- Uchambuzi wa Sera
Contact Info
+255 782 317 434
policy1@policyforum.or.tz
Education
Shahada ya Uzamili ya Sera za Maendeleo, Bradford University, UK
Mafunzo ya  Ufuatiliaji wa Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini.

Nicholas Lekule alijiunga na Policy Forum mwaka 2013 kama meneja anayehusika na uchambuzi wa Sera. Ana uzoefu zaidi ya miaka kumi akifanya kazi na Asasi za Kiraia nchini Tanzania. Nicholas anaratibu kazi za Kikundi Kazi cha Bajeti (BWG) ambacho huleta  pamoja AZAKI ambazo kazi zake zinazingatia uchambuzi wa sera na bajeti katika kiwango cha kitaifa na Kikundi Kazi cha Haki ya Kodi  (TJWG) ambacho huangazi masuala ya kikodi nchini.

Nicholas ana uzoefu mkubwa katika eneo la usimamizi wa fedha za umma / utawala bora. Kwa miaka kadhaa sasa amehusika katika uchambuzi wa sera za umma pamoja na bajeti, miswada inayohusiana na ufadhili wa miradi ya umma na kushirikiana na watunga sera kwa lengo la kuboresha michakato ya sera ili kuhakikisha kuwa sera zilizopo pamoja na zile ambazo zinafanyiwa kazi zinaboresha maisha ya watu. Kwa miaka mingi ya kufanya kazi na watunga sera, ameona maboresho katika michakato ya sera na thamani ya AZAKI. Nicholas ana shahada ya uzamili katika masuala ya Sera za Maendeleo inayotolewa na Chuo Kikuu cha Bradford. Yeye pia ni mhitumu wa mafunzo ya  Ufuatiliaji wa Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini.