![](/sites/default/files/team/HAitham%20fn.jpg)
Haitham Kichwabuta amejiunga na Policy Forum kama Afisa wa Tathmini, Ufuatiliaji na Kujifunza (MEL) anayehusika na kuongoza shughuli za MEL katika shirika. Kwa zaidi ya miaka minne, Haitham amekuwa akifanya kazi katika masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini katika sekta za mazingira, kilimo na afya ya umma. Ana ujuzi wa kina na uelewa wa usimamizi wa miradi, ufuatiliaji na tathmini na anauzoefu wa kuripoti kwa wafadhili tofauti wakati akifanya kazi na Oxfam nchini Tanzania na kampuni ya ushauri kabla ya kujiunga na PF. Haitham ana shahada ya Sayansi ya Mazingira na Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Miradi, Ufuatiliaji na Tathmini ya Afya inayotolewa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.