Muswada wa Bajeti, 2014

Categories

Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa sheria ya bajeti kwa lengo la kuweka mfumo wa kisheria utakaosimamia mchakato wa bajeti ya serikali kuanzia uandaaji, uidhinishaji, utekelezaji, ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa.

Muswada huu unakusudia kuweka mfumo bora wa kiutendaji kati ya serikali, bunge na vyombo vingine vinavyohusika katika mchakato wa bajeti, kuwepo kwa nidhamu ya bajeti kwa kuweka misingi ya kuzingatia mipango, mapato na matumizi, kuwepo kwa bajeti inayoaminika yenye kuzingatia utekelezaji kama ilivyoidhinishwa na Bunge pamoja na kuweka utaratibu maalum wa kufanya uhamisho wa fedha. Aidha, muswada huu unatarajia kujumuisha bajeti za wakala na taasisi za serikali katika vitabu vya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ili kuonyesha uwazi wa bajeti zao na jinsi zinavyochangia katika kukua kwa uchumi wa taifa.

Kuusoma Muswada Mpya wa Bajeti 2014, bofya 1 na 2

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter