Muongozo kuhusu muundo, utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya wilaya

Categories

Kwa mujibu wa Kifungu cha 18 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, Tume inawajibu wa kuunda Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume. Muundo wa Mabaraza ya Katiba unapaswa kuzingatia mgawanyiko wa kijiografia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mabaraza ya Katiba yatawashirikisha na kuwakutanisha wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii kwa lengo la kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba. Aidha, kifungu cha 17 (8) kinaeleza kuwa, isipokuwa kama mazingira yatahitaji vinginevyo, Tume itabuni utaratibu unaofanana ambao utatumika kila upande wa Muungano.

Kifungu cha 18 (6) kinaeleza aina nyingine ya Mabaraza ya Katiba kwa kueleza kuwa Tume inaweza kuruhusu Asasi, Taasisi au Makundi ya Watu kuwasilisha maoni yao kuhusu Rasimu ya Katiba.

Endelea kusoma...

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter