Mjue Diwani

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue
Diwani” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa kikundi kazi cha serikali
za mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii.
Lengo la kitabu hiki ni kuwasaidia madiwani kujua majukumu yao, wajibu
wao, mamlaka yao na mipaka yao na hatimaye waweze kuwatumikia
wananchi kwa ufanisi na uadilifu. Pia kitabu hiki kinalenga kuwaelimisha
wananchi kuhusu wajibu, mamlaka, majukumu na mipaka ya madiwani ili
waweze kudai uwajibikaji kutoka kwa madiwani pale ambapo uwajibikaji
unakosekana.
Kitabu hiki sio mwongozo wa madiwani bali ni kitabu cha jamii ambacho
kinaweza kumsaidia Diwani kujitambua na kuwasaidia wananchi kumfahamu
Diwani. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo wa maswali na majibu, kwa
lugha rahisi na katuni ili kumsaidia mwananchi wa kawaida kabisa kwenye
jamii kuelewa dhana mbalimbali zilizowekwa kwenye kitabu hiki.
Maudhui ya kitabu hiki yanatokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, 1977, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya
287, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, Sheria
ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, na Kanuni za Maadili na
Mwenendo wa Madiwani (Tangazo la Serikali Na. 280 la mwaka 2000).
Kitabu hiki kinaeleza maana ya Diwani, aina za madiwani, jinsi Diwani
anavyopatikana, sifa za kuwa Diwani, majukumu ya Diwani na maadili ya
Diwani. Kusoma zaidi bofya hapa

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter