Maonyesho ya 2014 ya Bunge: Asasi za Kiraia Zaaswa kutoa Ufumbuzi

Categories

AZAKI zimesifiwa kwa mchango wao katika kuielimisha jamii ya Kitanzania juu ya masuala muhimu ikiwa ni pamoja mchakato wa katiba unaoendelea. Wameshauriwa, hata hivyo, kutoa ufumbuzi na ushauri kwa serikali juu ya masuala muhimu ya utawala badala ya kuikosoa tu serikali.

shauri hili lilitolewa na Mheshimiwa Naibu Spika, Job Ndugai katika Maonyesho ya saba ya AZAKI yaliofanyika tarehe 16-Juni 18, 2014 ambayo yaliandaliwa na Foundation for Civil Society kwa kushirikiana na TACOSODE, Policy Forum, SIKIKA na HakiElimu. maonyesho haya katika bunge yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya asasi za kiraia na wabunge.

Mhe. Ndugai alitumia mfano wa mechi ya soka katika kuelezea ushirikiano kati ya asasi za kiraia na serikali. "Ni wale tu ambao wapo ndani ya mchezo ndio wanajua jinsi gani mchezo wanaocheza ni mgumu. watazamaji (akimaanisha AZAKI) wanaweza kutoa njia tofauti za kufunga goli lakini  hawajui jinsi ilivyo vigumu kufunga goli hilo. "Alitoa wito kwa asasi za kiraia kujiweka katika viatu vya serikali wakati wanatoa ushauri. Hii, aliwahimiza, itasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizi mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACOSODE, Theofrida Kapinga, aliisifu serikali kwa kutoa nafasi kwa ajili ya AZAKi kushiriki katika utengenezaji wa sera za taifa, akirejea kwenye lengo la maonyesho hayo ambalo ni  ushirikiano mzuri kati ya AZAKi na serikali utapelekea kuendeleza mchakato wa maendeleo ya taifa.

Katika kufunga hotuba yake, Alex Ruchyahinduru, Meneja wa Mawasiliano na Uchechemuzi wa Policy Forum alimshukuru Mhe. Job Ndugai kwa maneno yake ya hekima na akamsihi kuwahamasisha Wabunge wengine kufanya kazi na asasi za kiraia. "Wasiwaone AZAKI kama wapiga makelele bali wadau muhimu wa kufanya nao kazi katika kufikia malengo ya maendeleo ya taifa."

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter