MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA SERIKALI ZA MITAA

Ndugu Msomaji, tunafurahi kwa mara nyingine kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Malengo ya Maendeleo Endelevu na Wajibu wa Serikali za Mitaa” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Jukwaa la Sera (PF-LGWG) kwa kuelimisha wananchi kuhusu sera za kitaifa na kimataifa zinazopaswa kutekelezwa na Serikali za Mitaa ili kuhamasisha ushiriki wa
wananchi kwenye masuala ya umma na kukuza uwajibikaji katika jamii.
Kitabu hiki kimetafsiri na kuchambua kwa lugha ya Kiswahili malengo 11 kati ya 17 ya Malengo Endelevu ya Dunia yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa Tarehe 25 Septemba, 2015. Madhumuni ya kitabu hiki ni kuongeza uelewa wa wananchi, mamlaka za Serikali za Mitaa, madiwani, wana AZAKI na wadau wengine kuhusu malengo tajwa ili kujua majukumu yao na kuwawezesha kuyatekeleza kwa
vitendo kwenye ngazi husika. Aidha inatarajiwa kwamba yoyote atakayesoma kitabu hiki atapata uelewa wa majukumu yake na mamlaka anayoifanyia kazi hivyo kutimiza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na uadilifu. Kusoma zaidi bofya hapa.

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter