Skip to main content

Dira: Policy Forum ni asasi huru yenye dhamira ya kuhusisha wananchi, asasi zisizo za kiserikali, na sekta zote zingine za jamii katika michakato ya uundwaji wa sera. Dhamira hii pia inahusisha kuwezesha hatua zote za michakato ya uundwaji wa sera zinaelimisha wananchi, zinakuza uwezo wao wa kujihusisha na zinaendeshwa kwa njia inayotoa nafasi ya uwajibikaji.

Mwongozo: Policy Forum inahamasisha asasi husika kufanya shughuli zake kwa pamoja ili kuwezesha michakato ya uundwaji wa sera zinazoyaboresha maisha ya wananchi, hasa wale ambao wako kwenye nafasi za kutojiweza na katika hali duni. Nia hasa ni kuwawezesha wao kujipangia mikakati na kuwapa nyenzo ambazo zitawafanya waweze kushiriki katika mabadiliko.

Madhumuni:

  • Kutathmini matokeo ya sera zilizotekelezwa; kuhakikisha wakati wa utekelezaji wa sera, uhuru unakuwepo kwa chombo kinachofanya uchambuzii; kuhakikisha kuwa matokeo ya uchambuzi yanapatikana kwa wadau wote husika hasa asasi na vikundi vya utetezi ili kusaidia ufanisi na ubora wa shughuli zao.

  • Kuhakikisha kuwa matokeo yote ya uchambuzi yanayotoka Policy Forum yanasambazwa kwa upana kwa waundaji sera, asasi, na wananchi kwa ujumla. Policy Forum pia itahakikisha upatikanaji wa matokeo hayo ni wa rahisi, na unasaidia watumiaji walengwa.

  • Kuhakikisha asasi husika zinawezeshwa zaidi kuelewa, kuchambua, na kujihusisha kiufanisi katika ufanikishaji wa kushawishi michakato ya uundwaji wa sera za kitaifa na za ngazi za chini.

  • Kuhakikisha Policy Forum inahusika kikamilifu kama mtandao katika michakato ya uundwaji wa sera za kitaifa kwa mfumo maalum (kwa kutilia maanani vipengele ambavyo vitawezesha ushiriki uliyo bora zaidi, na kuhusika katika sehemu ambazo matokeo yanategemewa kuzaa matunda zaidi).