<p>Hiki ni kijitabu kidogo kilichoandiliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa ajili ya Elimu ya Uraia kwa watanzania wote. Kitabu hiki kinaelezea Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 kwa lugha rahisi ili kutoa fursa kwa wananchi kuelewa mambo muhimu yaliyomo katika Rasimu.</p>