Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya Policy Forum ya Mwaka 2014

Categories

Policy Forum ilichagua Bodi yake mpya ya Wakurugenzi wakati wa Mkutano wake wa mwaka wa 2014 uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili. Wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao, ni Hellen Kijo Bisimba - Legal and Human Rights Centre (LHRC), Nemence Iriya – Macsnet, Aida Kiangi – ActionAid Tanzania and Godfrey Wawa- Forum Syd hao ndio waliostaafu katika mkutano huu mkuu wa mwaka na kuwaacha nyuma Israel Ilunde-Youth Partnership Countrywide (YPC), Martina M. Kabisama-SAHRINGON and Betty Missokia / Godfrey Boniventura - Hakielimu kukaa kwa mwaka mwingine ili kuwe na uwiano kati ya uingizwaji na mwendelezo wa Bodi.

Katika hotuba yao ya kuondoka waliwashukuru wanachama wa PF kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kutumika katika bodi na ushirikiano wao wakati wa uongozi wao na waliwatakia Bodi mpya ya Wakurugenzi kila la kheri katika kufanyia kazi nzuri ya mtandao na kuiongoza Sekretarieti.

Wajumbe Wapya wa Bodi

1. Nancy Kaizilege-United Nations Association Tanzania (UNA-Tanzania)

2. Ibrahim Kabole/Fidelis Paul-WaterAid Tanzania

3. Paul Daniel - Care International

4. Jimmy Luhende-Action for Democracy and Local Governance (ADLG)

Wajumbe wa Bodi wanaokaa kwa mwaka mwingine

5. Israel Ilunde-Youth Partnership Countrywide (YPC)

6. Martina M. Kabisama-SAHRINGON

7. Betty Missokia / Godfrey Boniventura - Hakielimu

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter