Prisca Kowa ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alipata shahada yake ya Elimu ya Jamii, 2009. Kwa sasa anamalizia masomo yake ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Prisca alijiunga na Policy Forum kama Msaidizi wa Programu-Uwezo na Uwezeshaji 2011 kisha 2018 aliongezewa majukumu na kuwa Afisa Programu Mwandamizi Serikali za Mitaa na Uhusinao na Wadau. Amefanya kazi na CARE International na Aga Khan Foundation, akijihusisha na mambo ya jamii. Prisca anapendelea kujihusisha na mambo ya uchambuzi wa sera na kazi za jamii kwa ujumla.
Hellen Massawe alijiunga na Policy Forum 2017 kama Afisa Programu Msaidizi- Uchambuzi wa Bajeti na Sera. Ni mhitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata shahada ya Sheria. Baada ya kupata shahada ya sheria alijiunga na Shule ya Sheria Tanzania na kuhitimu mwaka 2017. Hellen hupendelea kujishughulisha na mambo ya kimaendeleo.
Amne Islam | Afisa Programu-Ufuatiliaji na Tathmini (MEL)

Amne Hamid alijiunga na Policy Forum kama Afisa wa Ufuatiliaji na Tathmini (MEL). Amne ana jukumu la kuongoza shughuli za MEL ndani ya shirika. Amne ana uzoefu wa zaidi ya miaka 3 katika tasnia wa MEL na ana shahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa. Ana uzoefu wa kubuni mifumo na mipango ya MEL kuandaa zana za kukusanya taarifa, kuhakikisha ubora wa taarifa, kufanya uhakiki wa miradi na kufundisha watumiaji wa mfumo wa MEL. Ana uzoefu wa kufuatilia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya elimu ya vijana, jinsia na afya za uzazi na ujasiriamali. Amepata ujuzi huo baada ya kufanya kazi na wafadhili kama vile SIDA, UNICEF, DFID, Novo na Global Fund. Pia amefanya kazi na Restless Development and Population Services International (PSI). Amne anatamani kuona MEL ikifanya kazi kwa ufanisi ndani ya Policy Forum.
Elinami John | Meneja-Uchechemuzi na Ushirikishaji

Elinami John alijiunga na Policy Forum, 2016. Kabla ya hapo alikuwa Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). Alikamilisha shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Ana shahada ya Uzamili katika masomo ya mawasiliano na habari kutoka Chuo Kikuu cha Karlstad, Sweden. Anapendelea kuchunguza mienendo na maendeleo ya utandawazi wa vyombo vya habari na mawasiliano na athari zake kwa jamii. Anatamani kuona Serikali ikitumia rasilimali kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya wananchi.