<p>Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja kati ya nchi tano zinazounda Jumuiya ya Afrika mashariki. Ipo kati ya Latitudo 1 na 12 kusini na Longitudo 29 na 41 Mashariki. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa na Tanzania bara na Zanibar kutokana na muungano wa mwaka 1964 wa Tanganyika na Zanzibar.</p>