Wafanyakazi Wetu

 • Richard Angelo
  Meneja- Uwezo na Uwezeshaji
   

  Richard Angelo ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alimaliza shahada yake ya Sanaa na Jamii mwaka 2006, Kabla ya kujiunga Policy Forum alifanya kazi shirika la HakiElimu kama mkufunzi na mshauri katika kitengo cha mawasiliano. Alijiunga na Policy Forum mwaka 2008 kama Msaidizi wa Programu-Habari, Mawasiliano na Uchechemuaji na sasa hivi ni Meneja wa Uwezo na Uwezeshaji. Anapendelea kuandika na mambo ya maendeleo ya jamii.

 • Nicholas Lekule | Meneja-Sera na Uchambuzi wa Bajeti

  Nicholas Lekule alijiunga na Policy Forum Mei 2013 katika nafasi ya Meneja wa  Uchambuzi wa Sera na Bajeti. Kabla ya kujiunga na Policy Forum, awali alifanya kazi katika shirika la Sikika kama Afisa wa Programu, nafasi ambayo aliishika kwa miaka mitano. Uzoefu wake ni katika eneo la uchambuzi wa bajeti na utawala kwa ujumla. Nicholas ana Shahada ya Sanaa katika Sosholojia aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007. Pia alihudhuria kozi kadhaa za muda mfupi ndani na nje ya nchi ili kuweza kuboresha ujuzi wake. Anapendelea kuona sera zetu zinafanya kazi kwa ajili ya watanzania wengi.

 • Semkae Kilonzo
  Mratibu
   
   

  Semkae Kilonzo alianza kazi Policy Forum mwaka 2007 kama Meneja anayehusika na habari, Mawasiliano na Uchechemuaji katika ofisi za mtandao wa sekretarieti, Sehemu ya matamanio yake ni kuona taarifa za uchambuzi wa sera zina sambazwa ipasavyo kwa watengeneza sera,asasi za kiraia na raia wote kwa ujumla. Na kwa sasa ni Mratibu, anayeongoza sekretarieti. Semkae ana shahada ya uzamili katika uandishi wa habari na masomo ya habari katita chuo cha Cardiff, Uingereza na kupata mafunzo ya habari Dublin Ireland na Shule ya Uandishi wa Habari Tanzania, Anapendelea kuhimiza watu wote kujihusisha katika shughuli za zote kutengeneza sera.

 • Rashid Kulewa
  Dereva
   

  Rashid Kulewa alijiunga sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2010, Alimaliza kozi yake ya komputa ICL Training Centre na amefanya kazi na mashirika tofauti kama FHI amabapo alikuwa kama dereva na Axios Foundation kama dereva na msaidizi wa afisa mgavi. Rashid anapendelea kuona watu wa Tanzania wanafaidika na mali asili za nchi yao.

 • Gibons Mwabukusi
  Meneja wa Utawala na Fedha
   

  Gibons Mwabukusi alijiunga Policy Forum mwaka 2010 kama Afisa Utawala na Fedha.Kabla ya kujiunga na Policy Forum alifanya kazi na mashirika tofauti yasiyo ya kiserikali katika mambo ya utawala na fedha. Ana stashahada ya juu ya uhasibu aliyopata kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania. Matamanio yake ni kuona Policy Forum ikiwa kipao mbele katika kuhamasisha utawala bora na uwajibikaji.

 • Amani Ndoyella
  Msaidizi wa Utawala
   

  Amani Ndoyella alijiunga na Sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2004 baada ya kumaliza masomo yake ya National Board for Materials Management (NBMM) Certificate. Na sasa hivi anahusika na utaratibu wa ugavi,orodha/hesabu za ofisi na kukatalogi taarifa muhimu kwa wanachama wa Policy Forum. Amani anapendelea kuona mali asili za Tanzania zinatumika ipasavyo ili kuleta maisha bora kwa watu wote wa Tanzania.

 • Nuru Ngailo
  Afisa Programu-Mawasiliano na Uchechemuaji
   

  Nuru Ngailo ameanza kazi Policy Forum mwaka 2011 kama Msaidizi wa Programu-Mawasiliani na Uchechemuaji, Ana shahada ya Sheria ambayo ameipata chuo cha Kishirikishi cha Tumaini, Iringa ambapo alihitimu mwaka 2010.Matamanio yake ni kuona watu wa Tanzania wana sauti kubwa katika mchakato mzima wa kutengeneza sera.

 •  
   
 • Prisca Kowa
  Afisa Programu-Uwezo na Uwezeshaji
   

  Prisca Kowa ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alipata shahada yake ya Sanaa na jamii mwaka 2009. Kabla hajajiunga na sekretarieti ya Policy Forum kama Msaidizi wa Programu-Uwezo na Uwezeshaji mwaka 2011, alifanya kazi na CARE International na Aga Khan Foundation,Katika mashirika yote alijihusisha na mambo ya jamii.Prisca anapendelea kujihusisha na mambo ya uchambuzi wa sera na kazi za jamii kwa ujumla.

  Anna Ndesamburo | Msaidizi wa Programu-Sera na Uchambuzi wa Bajeti

   
   

  Anna alijiunga na Policy Forum mwaka 2014 baada ya kufanya kazi kama “intern” wa Kampeni ya mama misitu. Ana digrii ya Utalii kutoka Tumaini University-Iringa na ana shahada ya  Jinsia aliopata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Na sasa ni Msaidizi wa programu ya Sera na Uchambuzi wa Bajeti katika sekretarieti Policy Forum.

Swahili